Tuesday, May 11, 2010

Happy birthday Nendeze


Bila shaka ulishawahi kukumbana na vibao kama "Usiamshe" na kingine kama "chance" kutoka kwa mwanadada Tecla aka nendeze enzi hizo akiwa Agees records. Pia ameshafanya chorus kwenye nyimbo nyingi tu maarufu, zikiwemo "binti kisura" ya  inspector haroun , "Jeshi la mtu mmoja" ya Fid q na "Nyeti" ya wagosi wa kaya

Tecla kituli ni msanii wa pili baada ya nikki mbishi kuanguka sahihi katika label ya music lab katikati ya mwaka jana. Je tukimwita Music lab first lady utabisha? nahisi utakuwa pamoja nami.

Akiwa music lab, nendeze ameshatoa kibao kimoja kikijulikana kwa jina la "BOY" ngoma ambayo ilibamba sana mwishoni mwa mwaka jana.


Kwa sasa mwanadada huyu ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha Tumaini-Dar es salaam akichukua Bachelor of Mass communication na leo hii ni siku yake ya kuzaliwa akifikisha miaka 23.

Happy birthday Nendeze

2 comments:

Anonymous said...

Happy B'DaY lvlY..

beric said...

Happy birthday mdada!
Rock the world, ningependa sana kama ungetengeneza nyimbo zenye theme zaidi ya moja! Talk abou other thngs in lyf, like encouragement, youth life, education, etc! Kwa kuwa wewe ni msomi, i hope u cn come up with alot of ideas in your music,
otherwise, try reading books za philosophers, hutakosa cha ku2nga!