Tuesday, February 9, 2010

JK ndani ya mpango mzima katika Tamasha la Malaria -ZINDUKA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete atahudhuria katika tamasha kubwa kabisa la uhamasishaji wa kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini litakalofanyika katika viwanja vya leaders tarehe 13 February 2010.

wasanii mbalimbali watajumuika pamoja kutoa burudani na kuhamasisha wananchi kupambana kwa dhati kutokomeza ugonjwa huo hatari unaoaminika kuongoza kupoteza maisha ya watu wengi duniani.

wasanii zaidi ya kumi na tano walijumuika kwa pamoja kuimba mwimbo moja kama njia ya uhamasishaji. Baadhi yao wakiwa ni marlaw, banana, mwasiti, lina, dito,prof j, amin, barnaba, grace matata, madee,keisha,jessica honore,mataaruma na msanii mkongwe Bi. kidude. Track hiyo ilifanywa chini ya supa dupa producer DUKE ndani ya music lab.

MLAB inatoa pongezi kwa wahusika wote wanaofanikisha kampeni hii.

No comments: