Thursday, November 26, 2009

Nyuma ya Pazia la Uhunzi ndani ya mLAB


mLAB pengine imebarikiwa kuwa na uwanja mkubwa sana wa wahandisi wa mziki (production crew) ikiwepo chini ya mhunzi mwenye uzoefu katika nyanja hii ya kazi za uhunzi wa milio (audio creactivity) maarufu kwa jina la DUKE aka DUKETACHEZ.

Duke amefanya kazi nyingi lakini maarufu zilizopata utambulisha mkubwa ni kama wimbo I'm Proffesional na ripoti za Mtaa za Farid Kubanda (FID Q), Traveller ya Msafiri Kondo(Solo Thang), Zero ya mwanadada Witness (member wa zamani wa kundi la WAKILISHA). Ndani ya Mlab, mkali huyu kashapeleka hewani nyimbo kama PUNCHLINES ya Nikki mbishi, Oh Boy ya Nendeze na Binti Kibiti wa Musa Vipaji Vingi feat Mataaruma

Ndani ya music laboratory, Duke ni head of production na pia ni sehemu ya wamiliki wa studio hizi. anazungukwa na wahunzi wengine chipukizi lakini wenye mambo makubwa kama Willie aka Mr. High Definition (HD), Texaz, Otuk na OX.

Willie ama HD ana uwezo mkubwa sana wa kupiga Piano,keyboard, bass,solo & Rhythim guitar. amejikita sana katika midundo ya Pop,rocky, Afro-pop, RnB, RnB hiphop, African vibes na gospel music. moja ya vielelezo vya kazi yake, ni inyimbo iliyo juu katika nyanja ya muziki nchini unaojulikana kama WIMBO WANGU wa msanii chipukizi alie chini ya labo ya mLAB akijulikana kama Grace Matata . HD pia hutumika sana na  supa dupa producer DUKE katika kulainisha zile hardcore hiphop bits za mtu mzima ili wale dada zetu pia wapate fleva za ki Rnb ndani ya mawe mazito.

Kama kweli we ni mpenzi wa soul na Hiphop basi kama utapata nafasi ya kuwepo kwenye session ndani ya studio za music laboratory, na TEXAS akawa kwenye machine...nina hakika kabisa hutotaka kubanduka mpaka nguli huyu chipukizi atakapotoka kwenye console..ana viji utamu vinavyoendana na beats za 9th wonder(blog itawaletea series za interviews ikiwemo ya huyu jamaa)....kazi zake bado kusikika masikioni mwa watu ila zipo za kutosha kabisa ikiwepo nyimbo moja @untitled" ya Teckla nendeze na nyingine ya "maisha haya" ya Grace Matata ambayo kuna tetesi huenda ikawa featured na mtu mzima Proffessor J kutegemeana na schedule ya Mr. heavy weight MC.

licha ya uhunzi na ubumbaji wa mziki, OTUK ni RnB singer alie chini ya lebo hii. ni mzuri sana katika ugongaji wa keyboard na Piano, akiwa amejikita sana katika production za RnB and soft hiphop zenye test ya kisasa zaidi huyu jamaa nadhani akikaa na Mr blu wanaweza tengeneza album la ajabu mazee. nyimbo yake aliyoifanya kwa ushirikiano wa DUKETACHEZ na OX inatarajiwa kulipuliwa tarehe 28th November 2009. tega sikio kwenye radio mbali mbali, kusikiza kazi ya mikono yake huyu jamaa.

OX ni habari ingine ambayo  nadhani kuanzia mwakani, pale mizigo iliyopo stock itakapoanza kushushwa kwa mahewa basi balaa lake sina hakika litazimwa na nani. yupo simple sana katika kazi zake lkn zinapomalizika unakuwa unashindwa kuelezea ubora wa prodidi hizo ukilinganisha na ethics zake za kazi.

ukiachana na nguli hao watano, pia mLAB inafanya kazi kwa ukaribu kabisa na producers wengine chupukizi na wazoefu waliopo dar na nje ya mkoa huu mkuu kibiashara. Amba aliepo iringa pia ni mfano wa producer wanaofanya kazi kwa ukaribu na studio hii, pia Abeid na Bosile wa Nairobi Kenya waliojikita sana na upande wa gospel music.
2 comments:

essau said...

Www.tzwap.wen.ru

Anonymous said...

Poa sana Kaka track moja ngapi?Ninampango wa kuja kugonga ngoma moja hapo.