Melody tamu inayoanza taaaaratibu! ni maneno yanayosikika mwanzoni kabisa mwa wimbo ulioshika chati hivi karibuni katika Radio mbali mbali hapa nchini "WIMBO WANGU". Hii ni sauti tamu na ya kipekee ya mwanadada mpya kabisa katika fani ya uimbaji nchini Tanzania akitambulika kwa jina la Grace Matata.
Mwanadada huyu ambae pia anacharaza guitar, ana uwezo mkubwa sana wa kupangilia nyimbo zake (composer) kuanzia utunzi, melody atakayoimbia na hata melody ya bit. Hivi unaweza kuamini kuwa MWIMBO WANGU ulikuwa composed na yeye mwenyewe kupitia gita lake halafu mzee mzima Willie HD akafata mawimbi ya melody hiyo akiyabadilisha kupitia piano yake na mwisho wa siku Duketachez akasema na zile Kick na snare zake za kipekee! kama hufahamu basi ndivyo songi hilo lilivyochangiwa na UTATU huo!
Grace hivi karibuni amejiunga mwaka wa kwanza na chuo cha usimamizi wa fedha IFM baada ya kumaliza elimu yake ya secondary katika shule maarufu ya Tambaza.
Mpaka kufikia sasa, Grace kashamaliza takribani nyimbo tisa huku akidaiwa na DUKE nyimbo7 kukamilisha nyimbo 16 na kuchujwa kufikia 12 zitakazo wakilisha album ya kwanza ya mwanadada huyu.
katika album hiyo, kutasikika sauti za wasanii wengine waliopo pia katika lebo ya mLAB kama Otuk, Darlington, Musa vipaji vingi na Njuu. Pia wasanii wengine ambao watasikika, ni pamoja na Mr. Blu aliechini ya zezzou Entertainment ambae soon anatarajiwa kuingiza vocal zake katika wimbo mmojawapo. Juhudi pia zinafanywa katika kuwapata wasanii wengine wawili watatu akiwepo Heavy weight MC, Professor J aka Dad kukamilisha mseto mzuri wa album hii.
Tarehe za release ya album hii bado haijawekwa bayana, ila ni matarajio kuwa album mpaka kufikia december mwishoni itakuwa imeshakamilika na pengine january single ya pili itaachiwa kwa mahewa pamoja na video yake
No comments:
Post a Comment