Wednesday, December 30, 2009

Huku Traditional Kule Dansi

Sasa ni zamu ya Lapakache ku introduce kazi mbili zenye mahadhi tofauti kutoka kwa wazee wa shoka ACHIGO BAND na yule jamaa wa AfriJazz Musa vipaji vingi!

Kama mambo yakienda sawa, basi Achigo Band wataingia studioni wiki ijayo kurekodi vibao vyao viwili kwa mkupuo ambacho kimoja kinataraji kuingia hewani katikati ya mwezi january 2010. Ikumbukwe kuwa bendi hii ndio ile ile ya jemedari wa muziki alieko kifungoni The legendary Nguza Viking!

Musa vipaji vingi Tayari yeye kashafanya rekodi za kutosha, na wiki ijayo kuna ala nyingine tu za kunogesha pini hizo zitaongezwa kwa kushirikisha wakali kibao wa ala kutoka bendi tofauti tofauti za hapa nchini........ musa yeye anataraji kushusha pini mwanzoni mwa january sambamba kabisa na band ya Achigo.

Tunawaomba fans wote wa hawa majamaa wajiandae kupokea kazi nzuri na yenye ubunifu wa hali ya juu.

No comments: